Monday, April 11, 2011

HADITHI

Palikuwa na kijiji cha Mtunguchoya ,kata ya Legezamwendo,tarafa ya Madongokuinama,jamii ya zeruzeru, palikuwa na mzee mmoja aitwae mzee Toboamambo.Mzee Toboamambo alikuwa na watoto wawili Tototundu na Chongo.Mzee Toboamambo alichukiwa sana pale kijijini kwao kutokana na tabia yake ya kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na vyombo vya dora kwa kila ovu aliloliona pale kijijini, Viongozi wa halmashauri ya kijiji walimpenda sana mzee huyu kutokana na ushirikiano wake,Alikuwa mpenda maendeleo asiyeogopa kupigania maendeleo ya kijiji chake.Katika kijiji kile palikuwa na msitu mkubwa ulijulikana kwa jina la Takalang’onyo.